‎‎MENEJA MKUU GCU LTD, ARIDHISHWA NA MWITIKIO WA WAKULIMA KUUZA PAMBA. ‎

Na Mwandishi wetu.

‎MENEJA wa Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Geita (GCU LTD), Ramadhani Sadiki Sephu, amefanya ziara katika vituo mbalimbali vya ununuzi wa pamba wilayani Geita kwa lengo la kujionea mwenendo wa zoezi la ununuzi wa zao hilo na kuzungumza na wadau mbalimbali.

‎Katika ziara hiyo, Meneja Mkuu ameeleza kuridhishwa na mwitikio mkubwa wa wakulima ambao wanaendelea kuuza pamba yao kupitia GCU LTD, akisema hali hiyo inaonesha imani ya wakulima kwa chama hicho kutokana na huduma bora kinazozitoa.

‎Katika Ziara hiyo, Meneja Mkuu ameambatana na Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba Wilaya ya Geita Filbert Matondwa, ambapo wamesisitiza wanunuzi wote kuendelea kuzingatia viwango vya ubora wa pamba ili kuhakikisha zao hilo linakidhi matakwa ya soko na kuongeza thamani yake.

‎Kwa upande wao, wakulima waliozungumza wakati wa ziara hiyo wameeleza kufurahishwa na huduma zinazotolewa na GCU LTD, hususan malipo ya haraka na kwa wakati, jambo ambalo limewapa motisha wa kuendelea kukiuzia chama hicho pamba yao.

‎GCU LTD imeendelea kuhimiza wakulima kuzingatia kanuni bora za uzalishaji na utunzaji wa pamba ili kuongeza ubora wa zao hilo na kuinua kipato chao pamoja na kuchangia ukuaji wa sekta ya pamba nchini.

MWISHO.

Source:

Rubondo FM

Social network.




Post a Comment

0 Comments