Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao amefariki dunia leo Juni 20, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amethibitisha kifo Cha Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao, kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Akizungumza kuhusu msiba huo, Chacha amesema kifo cha kamanda huyo ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi na wananchi wa Mkoa wa Tabora kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha usalama na utulivu wa mkoa huo.
"Ni kweli amefariki dunia majira ya saa 6 mchana huu, katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa Matibabu takribani wiki tatu sasa, taarifa zaidi mtaendelea kujulishwa" amesema Mkuu wa Mkoa huo, kwa njia ya simu.
SACP Abwao alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kufariki dunia. Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ugonjwa wake pamoja na ratiba ya mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia yake pamoja na mamlaka husika.
R.I.P Kamanda Abwao


0 Comments