Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo Juni 2, 2026.

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

‎SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi, imesema inahitaji kiasi cha Shilingi Bil. 6.2 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi 792 ili kupisha ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Simiyu kinachotarajiaa kujengwa Igegu wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

‎Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile wakati akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kujua lini serikali itakamilisha Upembuzi yakinifu Kwa ajili ya kujenga uwanja wa ndege wa Mkoa wa Simiyu.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akijibu swali Bungeni leo Juni 2, 2026.

‎Mheshimiwa Tina Chenge, aliuliza "Kwa kuwa ni takribani miaka 10 sasa, tangu serikali itoe tamko la kujenga uwanja wa ndege wa Mkoa wa Simiyu, ni lini serikali itakamilisha upembuzi yakinifu Kwa ajili ya kujenga uwanja a Mkoa wa Simiyu?."  

‎Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema, "kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, nimjibu Mama Chenge, swali lake la nyongeza kuhusiana na uwanja wa ndege wa Mkoa wa Simiyu...Ni kweli kabisa sera ya serikali kujenga viwanja vya ndege kwenye mikoa takribani yote," amesema na kuongeza.


‎"Na kuonyesha umuhimu wa Mkoa wa Simiyu, tayari serikali imekwisha tambua eneo ambalo imekwisha kulipata Kwa Sasa tumetambua kwamba tunahitaji takribani shilingi Bil. 6.2 ili tuweze kulipa fidia Kwa wananchi wapatao 792, baada ya hapo tunaendelea, nimwombe Mhe. Chenge pamoja na Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, wawe wavumilivu kwani Serikali inakwenda kujenga Mradi huo muhimu hatua Kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha serikalini."

‎Mwisho.