MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, Nkenyenge Charles.

Na Mwandishi wetu.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, Nkenyenge Charles, ameongoza kikao cha Baraza la Madiwani cha cha robo ya tatu 2025/2026 kilichoketi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ulioko Nyaumata kwa ajili ya kujadili taarifa za Maendeleo za Kata.

Katika Mkutano  huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Nkenyenge Charles pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo, Iddi Ndabona ambaye alikuwa katibu wa Kikao hicho, ambapo Madiwani waliweza kuwasilisha  taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika kata kumi  zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi zilizotekelezwa katika kipindi cha robo ya tatu kati ya Januari hadi Machi 2026.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watendaji wa Kata 10 za Halmashauri ya Mji Bariadi Mkoani Simiyu.

Aidha, Baraza hilo litaendelea kesho kujadili taarifa za Kamati mbalimbali, maswali ya papo kwa hapo pamoja na kujadili masuala mengine yanayohusu Maendeleo ya Halmashauri hiyo.

Mwisho.