ALIYEKUWA mwanachama wa CCM, Peter Msigwa, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho na kurejea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kutafakari kwa kina kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki na utu wa binadamu yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Katika taarifa yake, Msigwa amesema hawezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya kutokana na yaliyotokea, hivyo ameamua kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za chama hicho.
Pia ameomba radhi kwa Watanzania na wanachama wa CHADEMA walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wake wa awali, akisema binadamu hukosea lakini dhamira inapozinduka ni muhimu kusimama upande wa haki, utu na demokrasia ya kweli.
Anaandika Peter Msigwa.
"Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki."
Asanteni Sana.


0 Comments