MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simelanga akizungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijiji cha Senta kata ya Masewa wilayani humo.MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simelanga ameahidi kutoa mifuko 200 ya saruji ili kuunga mkono Shughuli za Maendeleo katika vijiji vya Mwantimba, Senta, Igabanilo, na Nyamikoma kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa pamoja na ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mwantimba kata ya Masewa wilaya humo.
Akizungumza kwa nyakati mbalimbali kwenye mikutano ya kutatua na kusikiliza kero za wananchi, Simalenga amewapongeza wananchi hao kwa kujitolea nguvu kazi kujenga miundombinu ya Maendeleo huku akiisisitisa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi kuwaunga mkono ili kukamilisha ujenzi wa miradi yao.
"Hapa Mwantimba mna Mpango wa Kujenga zahanati ili kuwapunguzia akina mama umbali kwenda kujifungua na kupata huduma ya Afya, mimi naahidi Kuchangia mifuko 50 ya Saruji kuwaunga mkono...hapa Kijiji cha Senta mmejenga madarasa 4 nami nitawaunga mkono kwa mifuko 50 ya saruji, Igabanilo pia mifuko 50, Nyamikoma nitawapa mifuko 50 kujenga Shule nyuma ya mlima, Halmashauri tuonyeshe kuwaunga mkono" alisema Simalenga.
Katika hatua nyingine Simalenga aliwataka wananchi hao kitojihusisha na Ujangili huku akisisitiza kuwa serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imekuja na Mpango wa Kujenga uzio wa Umeme kandokando ya hifadhi ili kudhiti Tembo wanaovamia mkazi ya wananchi na kuharibu mashamba yao.
Afisa Wanyamapori wilaya ya Bariadi, Kwembea Seso alisema serikali wanaendelea kuleta vifaa vya kudhibiti Tembo ikiwemo magari, tochi pamoja na mabomu ya kudhiti wanyama hao.







0 Comments