
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi ya (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imepongeza kasi ya Ujenzi wa Barabara ya Kahama-Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 Inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa Ufadhili Migodi ya Barrick nchini ya Bulyanhulu na North Mara itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 101.2.Ujenzi wa barabara hii unatekelezwa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation.
Ujumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Kahama ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga ulitembelea mradi huo wa ujenzi wa barabara na kutoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals kwa kufanya uwekezaji unaoenda sambmba na kufanikisha miradi mikubwa endelevu inayobadilisha maisha ya wananchi kuwa bora ma itakayoacha alama ya kudumu hata kwa vizazi vijavyo.

Thomas Myonga
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga amesema wamefurahishwa kuona mradi huu mkubwa unaendelea vizuri na mkandarasi yupo kazini na kutoa rai rai kwa mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha mradi huu anakamilisha kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza na wananchi waondokane na kero waliyokuwa nayo ya ubovu wa barabara hii kwa muda mrefu.
Alisema ujenzi wa barabara hii ambao umefikia asilimia zaidi ya asilimia 70 ya utekelezaji wake ukikamilika utasaidia kukuza Uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Shinyanga na Geita “CCM katika Ilani yake ya Uchanguzi ya Mwaka 2025/30 inayosimamiwa na Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan iliahidi kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo hivyo mkandarasi anapaswa kuhakikisha inakamilika katika muda uliopangwa.

Mhandisi John Kalando
Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya Ujenzi , Mhandisi John Kalando kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) amesema tayari Kampuni ya Barrick nchini imeshalipa fedha zote kwa mkandarasi hivyo watahakikisha wanamsimamia ili ikamilike ndani ya muda.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, amesema kamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kuondoa adha ya vumbi kwa wakazi wa mji ya Segese, Lunguya na Kakola kutokana na barabara ya awali iliyokuwa na vumbi na kuwa katika hali mbaya ya kutopitika hali iliyokuwa ikiwasababishia hasara kubwa wasafirishaji na kuleta kero kubwa kwa wananchi.
Kutekelezwa kwa mradi huu mkubwa kwa mafanikio ni kielelezo kinachodhihirisha ubia wa Barrick na Twiga unavyofanikisha kuchochea utengenezaji endelevu wa thamani katika uchumi wa Tanzania na jinsi Serikali ikishirikiana na sekta binafsi inavyoweza kuleta matokeo chanya kwa kufanikisha miradi mikubwa endelevu ya kunufaisha wnanchi kwa kipindi cha muda mrefu.














0 Comments