WANUFAIKA MIKOPO YA 10% MASWA WAHIMIZWA KUREJESHA KWA WAKATI.

 

Mkuu wa wilayabya Maswa,Dk Vicent Anney (mwenye kipaza sauti) akikabidhi mfano wa hundi kwa kikundi cha watu wenye ukemavu wilayani humo. Picha na Samwel Mwanga


Samwel Mwanga, MASWA.

HALMASHAURI ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu  imetoa jumla ya Sh 98.7 milioni kwa vikundi 12 vya vijanawanawake na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa asilimia 10,huku wanufaika wakihimizwa kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati.

Kati ya fedha hizo vikundi vitatu vya vijana vimekopeshwa Sh32,5 milioni,vikundi nane vya wanawake vimekopeshwa Sh 57 milioni na kikundi kimoja cha watu wenye ulemavua wamekopeshwa Sh 9,2 milioni.

Akizungumza Machi 3,2026 katika hafla ya kukabidhi hundi iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Mkuu wa wilaya ya Maswa,Dk Vicent Anney amesema fedha hizo zimetafutwa kwa juhudi kubwa za ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya hiyo,hivyo zinapaswa kutumiwa kwa malengo ya kujikwamua kuichumi badala ya matumizi yasiyo na msingi.

Amesisitiza kuwa wanufaika wanapaswa kuwa na nidhamu ya matumizi  ya mipango thabiti ya biashara badala ya kupunguza mikopo kwa mahitaji ya kijamii kama sherehe na matumizi binafsi yasiyo ya uzalishaji.

Mkuu wa wilaya ya Maswa, Dk Vicent Anney akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijjana,wanawake na wenye ukemavu wilayani humo.

“Hii fedha ya mikopo si fedha ya sadaka ni lazima irejeshwe na ukiifanyia starehe na ukashindwa kuirejesha tutakukamata tu ili na watu wengine waweze kukopa na ndiyo maana mchakato wa utoaji mikopo kwa sasa unapitia ngazi mbalimbali za serikali ili kuondoa urasmu wa utoaji wa mikopo hii,”amesema.

Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Hollo Ngeme  amesema kuwa mikopo hiyo ambayo imetokana na mapato ya ndani huku vikundi vingi vikijishughulisha na shughuli kama vile ufugaji,usafirishaji,biashara na viwanda vidogo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Maswa,Hollo Ngeme akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijjana, wanawake na wenye ukemavu wilayani humo.

Amesema vikundi vyote vilivyopata mikopo walivitembelea na kuona shughuli wanazozifanya hivyo wakaona vinafaa kupata mkopo hatua ambayo inachochea ukuaji wa kipato chao.

Kwa niaba ya wanufaika, Nasibu Masele ambaye ni mlemavu kutoka Sola mjini  Maswa amesema kuwa mikopo hiyo itaongeza mitaji ya wajasilimali hasa kwa watu wenye ulemavu ambao mara nyingi katika jamii hawapewi nafasi kubwa katika shughuli za uzalishaji,

“Mie nafanya biashara ya kusafirisha mizigo kwa kutumia pikipiki na matairi matatu yaani guta na fedha nyingine nitaendeleza biashara yangu ya kondoo kwa maana kondoo ukiwalisha kwa muda mfupi watakupatia faida kubwa sana nah ii itaniwezesha kurejesha mkopo huu kwa wakati,”amesema.

Naye Yunice Mangengula wa Kata ya Nyalikungu  ambaye ni mnufaika wa kikundi cha wanawake amesema kuwa kikundi chao kinachojishughulisha na usafirisha wana uhakika wa kurejesha mkopo huo kwa wakati kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mzuri katika biashara yao wanayoifanya.

Munufaika wa vijana, John Jeje kutoka kikundi cha Mkombozi kilichopo katika kijiji cha Wigelekelo wilayani humo ameishukuru kwa mkopo huo na kuhaidi kutoa elimu kwa vijana wengine juu ya matumizi sahihi na umuhimu wa kurejesha mikopo kwa wakati.


MWISHO.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo katika halmashauri ya wilaya ya Maswa wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa mikopo.



Post a Comment

0 Comments