Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akijibu swali Bungeni.

Na Costantine Mathias, Dodoma.

SERIKALI imepanga kujenga kilometa 50 za lami katika Barabara ya Bariadi-Sibiti mpaka Singida ambapo Kuna mkandarasi anayesubiri kulipwa Malipo ya awali ikiwa ni pamoja na kujenga lami kwenye daraja la mto Sibiti upande wa Singida na Upande wa Simiyu. 

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge. 


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akijibu swali Bungeni.

Tina Chenge aliuliza, Kwa kuwa ni sera ya serikali kuhakikisha kila Makao Makuu ya mkoa yanaunganishwa kwa Barabara za lami, Je ni lini serikali itaanza kujenga Kwa kiwango cha lami Barabara ya kutoa Bariadi, Lagangabili, Mwanhuzi, Sibiti, Iguguno hadi Singida. 


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge. 


Mhandisi Kasekenya alimhakikishia Mbunge huyo kuwa serikali imepanga kujanga kwa kiwango cha lami kilomita 50 katika Barabara hiyo. 

Mwisho.