ASKOFU SANGU AWAHIMIZA WAKRISTO KUWA NURU NA MWANGA KWA WENGINE.


Akitoa homilia katika Misa ya Mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu, Mume wa Bikra Maria, Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga, Askofu Sangu amesema waamini wanapaswa kutumia maadhimisho ya Pasaka kama fursa ya kuanza upya maisha yao ya kiroho.

Amewasisitiza kuishi kwa kuakisi matendo mema kwa jamii, wakiongozwa na misingi ya imani na maadili mema.

Aidha, amewaasa kuepuka hasira na matendo maovu, ikiwemo uchochezi, ugomvi na imani za kishirikina, badala yake waongozwe na fadhila za unyenyekevu, utu wema na uvumilivu.

Pia amewakumbusha umuhimu wa kusoma Neno la Mungu mara kwa mara ili kuimarisha imani yao na kuishi kulingana na mafundisho ya Kristo, sambamba na kuwajali wenye uhitaji wakiwemo yatima, wenye huzuni na wafungwa.

Wakati huohuo, Askofu Sangu amewataka wakristo kusherekea sikuu ya Pasaka kwa amani na upendo, wakifuata maadili ya Kikristo

Wakristo duniani kote wameadhimisha Misa ya mkesha wa Pasaka, ambayo ni kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu Kristo, baada ya mateso, kusulubiwa na kifo chake msalabani, na hatimaye kufufuka siku ya tatu.

Askofu Sangu akiongoza Ibada ya Mwanga nje ya Kanisa.

Askoafu Sangu akiwasha mshumaa wa Pasaka nje ya Kanisa


Askofu Sangu akiwa akiongoza maandamano kuingia Kanisani baada ya kuwasha mshumaa wa Pasaka

Paroko wa Parokia ya Ndembezi Padre Richard Makoye akipiga mbiu ya Pasaka

Wanakwaya wakiwa kwenye Misa ya Mkesha wa Pasaka

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi (kulia mwenye Miwani)  na msaidizi wake akiwa kwenye Misa ya mkesha wa Pasaka Parokia ya Ndembezi

Baadhi ya waamini wa Parokia ya Ndembezi wakiwa kwenye Misa mkesha wa Pasaka

Baadhi ya wasomaji wa Masomo wakisoma masomo kwenye Misa ya Mkesha wa Pasaka katika Parokia ya Ndembezi

Askofu Sangu akiongoza sala mara baada ya somo kusomwa

Waamini wakiwa kwenye Misa ya mkesha

Askofu Sangu akitoa Homilia kwenye Misa ya Mkesha

Askofu Sangu akiongoza sala ya kubariki maji kwa ajili ya kuwanyunyizia waamini

Askofu Sangu akibariki maji kwa mshumaa wa Pasaka

SACP Magomi akiendelea na Misa ya Mkesha wa Pasaka

Askofu Sangu akiwabariki waamini kwa maji ya Baraka

Waamini wakimtolea Mungu sadaka

Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri Walei Parokia ya Ndembezi na Watawa wanohudumu katika Parokia hiyo,wakiwa kwenye Misa ya Mkesha wa Pasaka

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa salamu za Pasaka kwenye Misa ya Mkesha wa Pasaka. 


Post a Comment

0 Comments