KATI ya Novemba 28 na 30 2025, TAKUKURU (M) Geita ilipokea taarifa za uwepo wa vitendo vya rushwa vilivyofanywa na Cornel Lucas Magembe, Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini kwa kushirikiana na Frank Leonard Francis aliyekuwa Diwani mteule Kata ya Mganza.
Uchunguzi ulithibitisha kuwa viongozi hawa waliwakusanya madiwani wateule 20 wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika Hoteli ya Lakezone iliyopo Jijini Mwanza, baadaye Serengeti Palace Hoteli iliyoko Mji Mdogo wa Katoro-Geita, kwa lengo la kuwashawishi kwa hongo ya fedha, chakula na malazi ili kupiga kura za upendeleo kwa mgombea waliyemtaka katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Chato.
Source. UHURU DIGITAL.

0 Comments