MECHI YA TRA UNITED NA SIMBA YAAHIRISHWA.

 


Mechi ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba sports Club na Tra United iiyopangwa kuchezwa leo majira ya sa 16:30 imeahirishwa kutokana na Uwanja kujaa Maji kutokana na mvua kubwa iiyonyesha Mkoani Arusha. 

Bodi ya Ligi Kuu imehairisha mchezo huo kwa kutumia Kanuni ya 34:1(1.4) ya Ligi Kuu kuhusu Kuahirisha mchezo na Kanuni ya 39:13 kuhusu Waamuzi, kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mkoani Arusha, hali iliyosababisha uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutofaa kwa matumizi ya mchezo huo kwa mujibu wa Kanuni.

Mwisho .


Post a Comment

0 Comments